Sasa Naweza Kuona Mbali by Mary N. Johnson


Song Lyrics


Sasa Naweza Kuona Mbali
by Mary N. Johnson

Album: Sasa Naweza Kuona Mbali


Nilifungwa sana duniani
Na anasa za mwovu shetani ooh
Bali neema ya Mwenyezi Mungu
Imenifanya kuona mbali
Kweli

Sasa naweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu
Ooh sasa naweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu
Nisomapo neno lake Mungu
Linanihimiza moyoni ooh
Usiogope furahia
Bwana yu na wewe milele ooh

Sasa naweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu
Ooh sasa naweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu
Nilikuwa kipofu rohoni
Lakini Yesu akanifungua uuuh
Nikaona mwangaza wa ajabu
Nikapata wokovu wa Mungu
Kweli

Sasa naweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu
Ooh sasa naweza kuona mbali
Kwa roho matkatifu wa Mungu
Ahadi zake Mwenyezi Mungu
Ni za kweli na ni Amina
Aliyetuahidi sisi
Hakika yeye atatimiza

Sasa naweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu
Ooh sasa naweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu

Jamaa sasa twaweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu

Wazee sasa Mwaweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu

Wakenya sasa twaweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu

Waafrika sasa twaweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu

Watu wote sasa mwaweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu

Ukiokoka waweza kuona mbali
Kwa roho mtakatifu wa Mungu


Related Video from YouTube



Song Ratings and Comments


rating 5.0 with 101 votes

0 favs

View My Favorites


no comments to show

Related Albums by Mary N. Johnson



More Song Lyrics by Mary N. Johnson